Header Ads

test

Agizo la Waziri Mwigulu Nchemba kuhusu wanaotetea mimba mashuleni, pia Ushoga



Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh.Mwigulu Nchemba kwa mara nyingine amesisitiza swala la mimba mashuleni ni dhambi na sio utamaduni wa nchi hii kukubaliana nalo. Pia serikali kupitia Rais Mh. John Pombe Magufuli wameshaweka msimamo kwamba hakuna mwanafunzi atakayepata mimba na akaruhusiwa kuendelea na masomo au kurudi tena kwenye shule za serikali, watu wanaopinga jambo hilo wasitumie nguvu kubwa kupinga bali wajenge shule zao wao watoe hiyo haki ya kusomesha wanafunzi wajawazito au wale ambao tayari wamejifungua na siyo kulazimisha serikali kufanya hayo.

Waziri Nchemba amesema kama kuna taasisi yoyote imesajiliwa nchini na inafanya kampeni za haki za ushoga basi atafuta usajili huo na watu wake kukamata na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
“Wanaotaka haki za ushoga watafute tu nchi yao nyingine ambayo inaruhusu mambo hayo wakakae huko, kama ni taasisi imesajiliwa kwenye nchi yetu tukaigundua inafanya kampeni ya haki hizo na bahati nzuri zinasajiliwa Wizara ya Mambo ya Ndani nitazifutia usajili wao…
…..na kama ni raia wa Tanzania anaendesha kampeni hizo tutamkamata na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria, na kama si raia amekuja kwenye nchi yetu kuja kuendesha haki hizo tutampa amri ya kuondoka ndani ya nchi yetu hatapata fursa hata ya kuchomoa chaji ya simu kwenye soketi ya umeme” amesema Nchemba.

Tangaza Nasi kupitia Dawatihurutz.blogspot.com

No comments