Header Ads

test

Rayvanny ameshinda tuzo ya BET 2017



Msanii wa Bongo Flava, Rayvanny kutoka WCB ameshinda tuzo ya BET kipengele cha Viewers Choice Best New International Act Artist.
Tuzo hizo ambazo zimegaiwa usiku huu mjini Los Angeles, katika ukumbi wa Microsoft Theater Centre, Rayvanny ambaye alikuwa akiwania tuzo hizo kupitia kipengele cha Viewer’s Choice Best New International Act amefanikiwa kuibuka kidedea.
Wasanii wengine ambao alikuwa akishindana nao katika kipengele hicho ni Dave (Uingereza), Amanda Black (Afrika Kusini), Changmo (Korea Kusini), Daniel Caesar, Remi na Skip Marley (Jamica).
Ujumbe wa Diamond Platnumz baada ya Rayvanny kushinda tuzo ya BET 2017 kama ‘Hatimaye leo Unakuja nayo Tanzania Dah! ðŸ˜­….Zaidi ya miaka mi 3 tunaenda na kurudi Patupu….Hakika Maisha Uvumilivu na kutokata tamaa…. BRING IT HOME BOSS!!! @babutale
THE BET Viewers Choice Best New International Act 2017 !!!!!!!!!!!!!
WOOOOOOOOOYOOOOOOOO!!!!!!!….. Nikishindwa kwa Mkono wa Kulia, ntatumia hata Mkono wa Kushoto…..ila lazma ifike @Wcb_Wasafi TANZANIA!!!! Chkua hiyo😛 #Wcb_Wasafi #WinningTeam!’



Tangaza Nasi kupitia Dawatihurutz.blogspot.com

No comments