Header Ads

test

Kauli ya CHADEMA kuhusu Lowassa kuitwa kwenye mahojiano Polisi



Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Waziri Mkuu Mstaafu,  Edward Lowassa amepata wito kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumtaka kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kesho Jumanne, saa 4 asubuhi kwa ajili ya mahojiano. 
Taarifa iliyotolewa na CHADEMA imesema kuwa  hajapewa maelezo wala ufafanuzi wowote kuwa mahojiano hayo yatahusu nini hasa.
CHADEMA wameeleza kuwa taarifa za awali zinaonesha kuwa mahojiano hayo yanahusishwa na kauli za Lowassa alizotoa katika nyakati tofauti hivi karibuni wakati akishiriki futari katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Kwenye vyombo vya habari leo Lowassa ameripotiwa akimtaka Rais Magufuli kuwaachia huru mashehe wa uamsho ambao inadaiwa wanashikiliwa kwa miaka minne sasa.
Tangaza Nasi kupitia Dawatihurutz.blogspot.com

No comments