Header Ads

test

Rayvanny wa WCB akamilisha wimbo wake na Jason Derulo



Msanii kutoka WCB, Rayvanny amekamilisha ndoto yake aliokuwa akiiota kwa muda mrefu.
Hitmaker huyo wa Zezeta na mshindi tuzo ya BET 2017, amefanikiwa kukamilisha kufanya kazi na Jason Derulo wa nchini Marekani.

Kupitia mtandao wa Instagram, Raymond ameweka picha akiwa syudio na msanii huyo na kuandika,“God bless you my brother @jasonderulo its amaizing opportunity,am so grateful for that……… Toka Saa 8 Usiku amekaa na mimi hadi Asubui… Studio kulikua na Watoto wakaaaaaliiiii ðŸ˜‚ lakini kawacha waondoke sababu walichoka kukaa studio yeye kabaki na sisi tu. Naamini kilichofanyika Mtakipenda. Thanks boss @afrikidd @babutale.”
Baada ya wasanii hao kukamilisha kazi yao hiyo walijumuika pamoja katika kucheza wa mpira wa kikapu ambapo Jason alioneshea umahiri wake wa kucheza mchezo huo dhidi ya Raymond. Wawili hao kwa mara ya kwanza walikutana nchini Kenya kwenye Coke Studio Afrika wiki chache zilizopita.

 Tangaza Nasi kupitia Dawatihurutz.blogspot.com

No comments