Header Ads

test

Victor Wanyama apewa mtaa Dar es Salaam, Wilaya ya Ubungo


Victor Wanyama akiwa na Meya wa Ubungo Boniface Jacob (Kulia)
Meya wa Manispaa ya Ubongo Boniface Jacob, amemtunuku mtaa, Kiungo wa Tottenham ya England Victor Wanyama raia wa Kenya.
Jacob ambaye ni Meya akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameonekana kufurahishwa na mchezaji huyo kufika katika eneo lake na kuunga mkono michezo.

Hivyo kwa kufurahishwa na namna alichofanya kiungo huyo Mkenya ambaye ni nahodha wa Harambee Stars ameamua kumzawadia mtaa utakao tambulika kwa jina lake.

Mtaa huo awali ulikuwa ukifahamika kwa jina la Viwandani kabla ya kubadilisha na kuitwa Victor Wanyama Street.
Kabla, Wanyama alihudhuria mashindano ya Ndondo Cup yanayoendelea katika Uwanja wa Kinesi Ubungo Shekilango jijini Dar es Salaam jioni hii.
Tangaza Nasi kupitia Dawatihurutz.blogspot.com

No comments