Okwi rasmi Simba, asaini kuichezea miaka miwili
![]() |
Okwi akisaini mkataba wa kuichezea Simba Sc |
Mshambuliaji Emmanuel Okwi amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea klabu ya Simba. Okwi amesaini mkataba huo jana usiku mbele ya Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' huku bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’ akishuhudia.
Okwi alitua nchini Jumamosi usiku akitokea kwao Uganda, kisha jana Jumapili akamalizana na klabu hiyo ambapo hii inakuwa mara yake ya tatu kucheza klabuni hapo.
Okwi alitua nchini Jumamosi usiku akitokea kwao Uganda, kisha jana Jumapili akamalizana na klabu hiyo ambapo hii inakuwa mara yake ya tatu kucheza klabuni hapo.
Kwa upande wa Okwi alisema amefurahi kurejea Simba na kuwaahidi mashabiki kutekeleza wajibu wake ili kuiwezesha timu yake kushinda makombe ya mashindano ambayo itakuwa ikishiriki lakini pia akimshukuru MO Dewji kwa kufanikisha uhamisho wake.
“Nimekuja kupambana na kuhakikisha tunachukua ubingwa … namshukuru sana bosi MO Dewji kwa kufanikisha huu uhamisho wa kuja Simba,” alisema Okwi.
“Nimekuja kupambana na kuhakikisha tunachukua ubingwa … namshukuru sana bosi MO Dewji kwa kufanikisha huu uhamisho wa kuja Simba,” alisema Okwi.
Post a Comment