Header Ads

test

BREAKING NEWS| WANAFUNZI 32 WAFARIKI KATIKA AJALI YA BASI KARATU


Ajali mbaya imetokea Karatu mkoani Arusha katika mlima Rhotia baada ya basi dogo la St. Lucky ya Arusha aina ya Coaster lililokuwa limebeba wanafunzi kutumbukia kwenye korongo na kusadikiwa kusababisha vifo kwa wanafunzi waliokuwemo ndani ya basi hilo.



Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema ajali hiyo imetokea baada ya basi hilo kuacha njia na kuingia katika bonde la mto Mlera ambapo maiti wamepelekwa katika Hospital ya Lutheran Karatu.

Kamanda Mkumbo amesema kuwa kati ya maiti hizo miongoni mwao wapo waalimu ni 2 dereva 1 na wanafunzi 29 ambapo wanafunzi wa kiume 11 na wasichana 18 nakufanya jumla yao kuwa maiti 32.
Wanafunzi na waalimu hao walikuwa safarini kuelekea Karatu kwenye shule ya Tumaini English Medium Junior Schools kufanya mtihani wa kanda wa majaribio ya kujipima uwezo kabla ya kufanya mtihani wa taifa wa darasa la saba wa Kanda.
Shule hizo mbili zimekuwa zikifanya utaratibu wao wa kawaida,
Taarifa kutoka katika hospitali ya Lutheran Karatu, kwa muujibu wa Mbunge Ester Mahawe aliyeko hospitalini hapo , ni kuwa maiti zilizopokelewa katika hospitali hiyo ni 32 hii ikiwa na maana , miongoni mwao waalimu wawili, dereva mmoja , na wanafunzi ishirini na tisa.



Tangaza Nasi kupitia Dawatihurutz.blogspot.com

No comments