Header Ads

test

RONALDO HAT-TRICK YAIWEKA PAZURI MADRID KUELEKEA CARDIFF



Katika mchezo wa  kwanza UEFA Champions League hatua ya nusu fainali kati ya Real Madrid na Atletico Madrid maarufu kama Madrid Derby uliopigwa usiku wa Jumanne ya Mei 3, 2017 katika uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid, Cristiano Ronaldo alifanikiwa kuifungia timu yake magoli matatu dhidi ya majirani zao Atletico Madrid

Ronaldo alifunga goli la kwanza dakika ya 10 baada ya kupokea krosi nzuri toka kwa Casemiro aliyomalizia kwa kichwa mbele ya beki wa Atletico Stefan Savic, goli la pili alifunga dakika ya 73 baada ya kupokea pasi safi toka kwa Benzema na goli lake la tatu la mchezo huo alifunga dakika ya 86 lililo tolewa assist na Lucas Vazquez. Mabao ya Ronaldo katika UEFA Champions League hatua ya nusu fainali uwanja wa Santiago Bernabeu yameiweka Real Madrid nafasi nzuri ya kuingia fainali ya mashindani hayo itakayofanyika katika jiji la Cardiff.

Hat-trick hiyo inamfanya Ronaldo kufikisha magoli 103 na hat-trick saba kwa UEFA Champions League huku akilingana na Messi wa Barcelona, wote wakiwa na idadi sawa ya kufunga hat-trick kwenye mashindano hayo.


Ronaldo akifunga goli la kwanza

Ronaldo akifunga goli la pili

Ronaldo akifunga goli la tatu

Kocha wa Real Madrid akisheherekea moja ya magoli ya Ronaldo

Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone





Video| Real Madrid 3 - 0 Atletico Madrid - Highlights & Goals| May 2, 2017

Tangaza Nasi kupitia Dawatihurutz.blogspot.com

No comments