Header Ads

test

RAIS MAGUFULI AKABIDHI MAGALI YA WAGONJWA KWA WABUNGE WATATU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa magari mapya ya kubebea wagonjwa kwa wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwasaidia wananchi wa maeneo yao ya ubunge.

Katibu Mkuu Kiongoozi Balozi John Kijazi amekabidhi magari hayo aina ya Land Cruiser Hardtop kwa niaba ya Rais Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mkoa wa Katavi Mhe. Ally Keissy, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora Mhe. Munde Tambwe na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga.


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiwa na  Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mhe. Ali Mohamed Kessy,  Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora Mhe Munde Tambwe akiwaonesha magari ya kubebea wagonjwa waliyopewa kama msaada toka kwa Rais Magufuli.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiwa na  Mbunge wa Nkasi Kaskazini Mhe. Ali Mohamed Kessy,  Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora Mhe Munde Tambwe akiwaonesha magari ya kubebea wagongwa wanayopewa kama msaaada toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017.

Mbunge wa Nkasi Mhe Ali Mohamed Kessy akiwa na gari la kubebea wagonjwa  alilokabidhiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ikiwa msaaada toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2016.

Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tabora Mhe. Munde Tambwe akiwa juu ya gari la kubebea wagongwa  alilokabidhiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ikiwa msaaada toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2016.

Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga akionesha ufunguo wa gari la kubebea wagongwa  na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ikiwa msaaada toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2016.


Tangaza Nasi kupitia Dawatihurutz.blogspot.com

No comments