Header Ads

test

UJUMBE WA MRISHO MPOTO BAADA YA KUTUKANWA KISA KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI



Kupitia ukurasa wake wa Instagram msanii Mrisho Mpoto ameandika ujumbe huo baada ya kupokea matusi mengi, kebehi, na maneno machafu juu ya mimi kuunga mkono utendaji wa Rais Magufuli. Nimekuwekea hapo ujumbe wote wa Mrisho Mpoto:

Nimepokea matusi mengi, kebehi, na maneno machafu juu ya mimi kuunga mkono utendaji wa Rais Magufuli, kitu ambacho nakiamini kuna "KUKUBALIANA KWA KUTOKUBALINA" lakini siyo kumtukana mtu mwingie siyo busara hata kidogo, kwakua tu hakusema au hakufanya ambacho nafsi yako ilipenda kusikia. Kilichonifanya niandike ujumbe huu ni kuwa nisiwekewe maneno mdomoni yakua nimesema Rais Magufuli ni Mungu, kwa wale ambao hawakuangalia sherehe za MEI MOSI jana, naomba niseme kuwa hayo maneno siyo kweli na yamebadilishwa kutoka kwenye ukweli wa niliosema, Mimi ni mtu mwenye hofu na Mungu siwezi kusema hivyo, kumekuwa na utamaduni ikitokea mtu anauunga mkono utendaji wa Rais kuna ibukuka kundi la wapinga Maendeleo na kuanza kutukana. Naomba ijulikane kuwa sababu za kumunga mkono Rais, yale niliyokua nayaongea huko nyuma naona yanafanyiwa kazi hivi sasa!! MRISHO MPOTO mpaka sasa namuunga mkono Rais MAGUFULI, Iwe nachumia tumnbo kama inavyosemwa au nimevimbilwa kwa shibe.
A post shared by mjombampoto (@mrishompoto) on

 Tangaza Nasi kupitia Dawatihurutz.blogspot.com

No comments