Anthony Joshua ashinda kwa KO dhidi ya Wladimir Klitschko Wembley
![]() |
Bondia Wladimir Klitschko akiwa chini baada ya kupigwa ngumi nzito na mpinzani wake Joshua. |
Anthony Joshua mwenye umri wa miaka 27 alifanikiwa kumpiga Wladimir Klitschko mwenye umri wa miaka 41 kwa Knocks Out katika raundi ya 11 ya mchezo huo. Kwa matokeo hayo yanamfanya Anthony Joshua kuweza kuitetea na kuweka rekodi zaidi ya kucheza mapambano 19 na kushinda yote 19 kwa Knocks Out. Pia upande wa bondia wa Ukraine Wladimir Klitschko huu unakuwa mpambano wake wa 5 kupoteza katika historia yake ya kucheza ngumi.
"[Mimi] 19-0, ndani ya miaka mitatu na nusu katika mchezo," Joshua alisema. "Kama nilivyosema, mimi sio mkamilifu, lakini hujaribu. Nafanya juhudi zaidi. Ndivyo ilivyo. Kama nilivyosema, kama hushiriki, hutaweza kujua matokeo."
Joshua vs. Klitschko ubao wa alama za pambano:
R1 | R2 | R3 | R4 | R5 | R6 | R7 | R8 | R9 | R10 | R11 | R12 | TOTAL | |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Joshua
|
10
|
9
|
10
|
10
|
10
|
8
|
9
|
9
|
10
|
10
|
TKO
|
95
| |
Klitschko
|
9
|
10
|
9
|
9
|
9
|
10
|
10
|
10
|
9
|
9
|
94
|
Post a Comment