Header Ads

test

EL CLASICO: MESSI SHUJAA BERNABEU, AWEKA REKODI MPYA YA MAGOLI



Magoli ya Lionel Messi dakika za 32, 93 na lile la Rakitic dakika ya 73 yaliiwezesha Barcelona kuondoka na pointi 3 muhimu katika mchezo wa El Clasico uliopigwa katika uwanja wa Santiago Bernabeu. Kwa upande wa Madrid magoli yao yalifungwa na kiungo Casemiro dakika ya 28 na lile lililofungwa na James Rodriguez dakika ya 83 aliyeingia kuchukua nafasi ya Karim Benzema. Real Madrid walipata pigo kubwa baada ya beki wao tegemezi Sergio Ramos kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 77 baada ya kumchezea madhabi Lionel Messi hivyo kuifanya Madrid kucheza pungufu dhidi ya Barcelona kwa dakika zilizobakia za mchezo huo. Magoli hayo mawili aliyoyafunga Messi katika El Clasico yanamfanya kufikisha idadi ya magoli 500 aliyoyafunga akiichezea klabu ya FC Barcelona na pia kufikisha magoli 23 aliyoyafunga katika El Clasico muda wote, huku akifuatiwa na Alfredo Di Stéfano mwenye magoli 18 na Cristiano Ronaldo mwenye magoli 16.

Vikosi vilivyo anza katika mchezo huo



Ramos akimchezea Messi madhambi

Ramos akionyeshewa kadi nyekundu na refa Hernandez
Messi akishangilia baada ya kufunga goli la pili



Messi akiwaoneshea mashabiki jezi yake baada ya kufunga goli la pili na la ushindi katika mchezo huo
Magoli 500 ya Messi akiichezea FC Barcelona
  Matokeo mengine ya michezo ya La Liga wikiendi hii:


Msimamo wa La Liga baada ya michezo ya 33:




Matukio na magoli ya mchezo wa El Clasico: 

Tangaza Nasi kupitia Dawatihurutz.blogspot.com

No comments