Header Ads

test

MANUKATO YA DIAMOND PLATNUMZ 'CHIBU PERFUME' KUUZWA BEI HII NCHINI KOTE



Leo mchana Diamond Platnumz amezindua rasmi bidhaa yake ya manukato yaitwayo CHIBU PERFUME ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na Watanzania hatimae bei yake yatangazwa rasmi katika uzinduzi huo uliofanyika GSM Pugu Mall.
Diamond Platnumz alikutana na waandishi wa habari kuzindua rasmi bidhaa hiyo ambapo amesema kwa sasa bidhaa hiyo itaanza kupatikana karibia mikoa yote kwa bei za rejareja na jumla.
Akitaja bei ya Perfume hizo Diamond Platnumz amesema itapatikana kwa Tsh 105,000/= bei ambayo sio kubwa sana kwa watanzania walio wengi.

Bidhaa hiyo kwa sasa itakuwa inapatikana katika maduka ya GSM Mall.

Tangaza Nasi kupitia Dawatihurutz.blogspot.com

No comments