Header Ads

test

BREAKING NEWS: KAGERA SUGAR WAREJESHEWA POINTI ZAO 3 NA TFF DHIDI YA SIMBA




Maamzi ya kamati ya katiba, sheria na hadhi za wachezaji imetangaza maamuzi yaliyofikiwa kupitia kwa Katibu mkuu wa shirikisho la soka Tanzania TFF Selestine Mwesigwa kuhusu Simba kupewa point 3 dhidi ya Kagera Sugar kwa madai ya kuchezeshwa mchezaji Mohamed Fakhi aliyedaiwa kuwa na kadi 3 za njano.
Baada ya kupitia ripoti na nyaraka mbalimbali, Kamati ya katiba, sheria na hadhi za wachezaji imeirudishia Kagera  Sugar pointi zake ilizokua imenyanganywa na Kamati ya Saa 72 kwa kuonekana imemchezesha mchezaji Mohamed Fakhi mwenye kadi 3 za njano.
Kamati ya Sheria imebani kutokuwepo kwa uhalali wa Kamati ya saa 72 kuwaalika (kuwashirikisha) watu walio nje ya kamati hiyo katika kikao hicho kilichofanya maamuzi ya kuipa Simba pointi 3.
Kufuatia kikao cha leo, matokeo ya mchezo kati ya Kagera Sugar dhidi ya  Simba yanabakia kama iliyokua awali, ambapo Kagera Sugar walishinda kwa mabao 2 – 1.
Aidha Kamati ya Sheria imeiagiza TFF kuwachukulia hatua wafanyakazi wa Bodi y  ligi walioshiriki katika kupotosha taarifa za mchezaji Fakhi mbele ya Kamati ya saa 72.

Tangaza Nasi kupitia Dawatihurutz.blogspot.com

No comments