Header Ads

test

TFF YAMFUNGIA MANARA NA FAINI MILIONI 9

Haji Manara
Kamati ya  Maadili ya Shirikisho la Mpira wa  Miguu Tanzania (TFF) imemsimamisha kutojihusisha na mpira wa miguu ndani na nje ya Tanzania kwa kipindi cha mwaka mmoja Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara.

Mapema wiki hii TFF ilimfungulia mashtaka Manara kwenye kamati hiyo inayoongozwa na wakili Jerome Msemwa kutokana na kauli alizozotoa wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya klabu ya Simba.
Uamuzi huo wa kumsimamisha Manara umetolewa leo mchana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili TFF, hali ambayo inampelekea kiongozi huyo kukaa mbali na soka kwa kipindi cha miezi 12.
Nje ya adhabu hiyo, Manara ametozwaa faini ya shilingi  milioni tisa za kitanzania.

Tangaza Nasi kupitia Dawatihurutz.blogspot.com

No comments