Header Ads

test

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA VIONGOZI WA SIMBA OFISINI KWAKE DODOMA


Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akijadiliana jambo na viongozi wa Klabu ya Simba Ofisini kwake Dodoma.
Waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe amekutana na uongozi wa Klabu ya Simba ya Dar es Salaam ukiongozwa na Rais wake Evans Aveva kwenye Ofisi zake Mjini Dodoma.

Uongozi wa Simba umeitikia wito wa Mhe. Mwakyembe wa kukutana naye na kujadili masuala mbalimbali ya mpira wa miguu zikiwemo fursa na changamoto katika mabadiliko ya maendeleo ya uendeshaji wa timu.

Aidha Mhe.Mwakyembe amepokea maoni ya Uongozi wa Simba na kushauri kuendelea kutoa ushirikiano na wadau wa mpira wa miguu nchini.

Kikao hicho pia kilihuduriwa na Katibu Mkuu wa Wizara husika Prof. Elisante Ole Gabriel, Mkurugenzi wa Michezo Yusufu Omary, Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja na Msajili wa vilabu na vyama nchini.


Mhe. Dkt Harisson Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na jopo la viongozi wa Simba waliofika ofisini kwake Mjini Dododma.


Tangaza Nasi kupitia Dawatihurutz.blogspot.com


No comments