Header Ads

test

WATU WASIOFAHAMIKA WAVAMIA MKUTANO WA CUF YA MAALIM SEIF



Watu nane wasiofahamika wamevamia mkutano wa wanachama wa CUF upande unaomuunga mkono, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad. 

Mkutano huo uliokuwa ukifanyika katika Hoteli ya Vina, Mabibo, ulipangwa kuanza leo saa tano asubuhi lakini kabla haujaanza watu waliovalia soksi nyeusi usoni(mask) walivamia na kuanza kuwapiga wanachama wa CUF na waandishi waliokuwa kwenye mkutano huo. 


Mtu mmoja miongoni mwa waliovamia mkutano wa wanachama wa CUF ameshambuliwa na wananchi wakati akijaribu kutoroka. 

Mmoja wa watuhumiwa wa uvamivi akiwa anapambana na wananchi

Mmoja wa watuhumiwa wa uvamivi akiwa kadhibitiwa baada ya kukatwa mguu na wananchi 

Mtuhumiwa akiugulia maumivu baada ya kukatwa mguu



Mtu huyo, ambaye hajafahamika alikuwa akitoroka pamoja na wenzake katika eneo hilo la Vina Hotel Mabibo mara baada ya kutekeleza uvamizi huo katika mkutano wa wanachama wa CUF.  Watu hao waliovamia mkutano huo, walikuwa na bastola.




Tangaza Nasi kupitia Dawatihurutz.blogspot.com


No comments