BREAKING NEWS: KAMATI YA SAA 72 YAIRUDISHA SIMBA MBIO ZA UBINGWA, YAIPA POINTI 3
Kamati ya Ligi ya masaa 72 iliyokaa kikao leo April 13,
2017 na kuamua kuhusu malalamiko ya Simba dhidi ya Kagera Sugar kumtumia mchezaji Mohamed Fakhi katika
mchezo wa April, 2 2017 huku akiwa na kadi tatu za njano kinyume na taratibu na
kanuni za Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Simba walipeleka
malalamiko hayo katika bodi ya Ligi na kuomba ipitie ripoti za waamuzi ili
kujulikana ukweli, leo April 13 kamati ya saa 72 chini ya mwenyekiti wake Hamadi Yahaya ilikaa
na kujiridhisha kuwa Kagera walikiuka taratibu hizo kwa mujibu wa
Kanuni, hivyo ikaamua kuwapa Simba
point zote tatu na magoli matatu kutoka mchezo huo dhidi yao. Simba imefikisha pointi 61 mbele ya wapinzani wao Yanga wenye Pointi 56.
![]() |
Mohamed Fakhi wa kwanza kushoto. |
Kamati
imejiridhisha kuwa mchezaji Mohamed Fakhi alioneshwa
kadi za njano katika michezo dhidi ya Majimaji, Mbeya City na African Lyon, hivyo hakustahili
kucheza katika mchezo dhidi ya Simba uliyochezwa April, 2 2017 katika uwanja wa Kaitaba na Simba ikapoteza
kwa magoli 2-1.
Msimamo
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya Simba kushinda rufaa yao dhidi ya
Kagera Sugar:
Post a Comment