Header Ads

test

Rais Magufuli awafukuza kazi watumishi 9932 wenye vyeti feki

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kuwafukuza kazi watumishi 9932 waliobainika wana vyeti feki huku akitaka wasilipwe mishahara yao ya mwezi huu.

Rais John Pombe Magufuli ameyasema hayo leo Ijumaa wakati akikabidhiwa orodha ya watumishi wa umma wenye vyeti feki na Waziri Angella Kairuki.
Alisema Rais Magufuli “Hizo nafasi 9932 zitangazwe ili wasomi hawa waanze kuziomba. Hawa wafanyakazi 9932 leo ni tarehe 28 ninajua wanajijua lakini na majina yao myaandike kwenye magazeti kwasababu ndiyo sera za uwazi, kama ulikuwa na baba yako ni kihio unamjua hapa moja kwa moja. Nataka watu wajifunze, wametuibia hela katika kipindi chote walichokuwa wakifanya kazi hawana qualification lakini wamekaa pale kwenye position ambazo hawastahili kuwepo hapo, hawa ni majambazi na majizi kama yalivyo majizi mengine kwasababu kwa vyoyote pefomance katika kazi zao hawakuweza kuperfom vizuri. Huwezi kuperform wakati huna qualification hio.”
Tangaza Nasi kupitia Dawatihurutz.blogspot.com

No comments