Header Ads

test

YANGA KUCHEZA MUDA HUU DHIDI YA MC ALGER NCHINI ALGERIA

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara na wawakilishi pekee toka Tanzania katika michezo ya vilabu ya kimataifa Dar es Salaam Young Africans wataingia uwanjani siku ya Jumamosi April 15, 2017 kucheza mchezo wa marudio kombe la Shirikisho la vilabu barani Afrika dhidi ya MC Alger nchini Algeria. Mchezo huo utachezwa mida ya saa 2:00 usiku kwa masaa ya Afrika Mashariki katika uwanja wa Stade 5 Juillet 1962, Algeria. 

Mchezo wa awali uliochezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam ambao Dar es Salaam Young Africans walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli mmoja pekee lililofungwa na kiungo Shabani Kamusoko.

Mwamuzi wa kati wa mchezo huo ni Yakhouba Keita kutoka Guinea na waamuzi wa pembeni ni Aboubacar Doumbouya na Mamady Tere wote kutoka Guinea. Mungu Ibariki Yanga, Mungu Ibariki Tanzania.
  






Tangaza Nasi kupitia [dawatihurutz.blogspot.com]





No comments