Header Ads

test

YANGA YAFANIKIWA KUTINGA NUSU FAINALI YA KOMBE LA FA




Mabingwa watetezi wa Kombe la FA maarufu kama Azam Sport Federation Cup Yanga wamefanikiwa kutinga nusu fainali ya Kombe hilo baada ya kuifunga timu ya Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya katika mchezo uliopigwa leo April 22, 2017 uwanja wa Taifa Dar es Salaam.  
Yanga wanaungana na timu za Simba SCAzam FC na Mbao FC kucheza hatua ya nusu fainali ya Kombe la Azam Sport Federation Cup msimu wa 2016/2017 baada ya kuiondosha Tanzania Prisons kwa jumla ya magoli 3-0, magoli ya Yanga yalifungwa na Amissi Tambwe dakika ya 15, Obrey Chirwa dakika ya 40 na Simon Msuva dakika ya 46.
Droo ya kupanga michezo ya nusu fainali ya Kombe la Azam Sport Federation Cup itachezeshwa kesho majira ya saa 9 Alasiri kwa kupanga nani atacheza na nani kati ya timu za Simba SCYangaAzam FC na Mbao FC ya Mwanza.

Tangaza Nasi kupitia Dawatihurutz.blogspot.com

No comments