Header Ads

test

HIZI HAPA MECHI ZA NUSU FAINALI UEFA CHAMPIONS LEAGUE






Draw ya mechi za nusu fainali katika ligi ya Mabingwa Barani Ulaya UEFA Champions League iliyochezwa mchana huu huko Nyon, Switzerland makao makuu ya UEFA imekamilika baada ya matokeo ya draw hiyo yakionesha Real Madrid kucheza na mahasimu wao wanaotoka jiji moja Atletico Madrid  yaani Madrid Derby pia FC Monaco kucheza na Juventus.




Real Madrid watawakaribisha Atletico Madrid siku ya Jumanne May 2, 2017 na FC Monaco ya Ufaransa watawakaribisha Juventus siku ya Jumatano May 3, 2017 katika michezo ya awali ya hatua hiyo. 



Michezo ya raundi ya pili itachezwa May 9, 2017 Juventus watawakaribisha Monaco pia May 10,2017 Atletico Madrid watawakaribisha Real Madrid. Mshindi wa mechi za FC Monaco na Juventus atakuwa mwenyeji katika mchezo wa Fainali utakaochezwa Cardiff June 3, 2017 katika uwanja wa Taifa wa Wales. 

Tangaza Nasi kupitia Dawatihurutz.blogspot.com




No comments