Header Ads

test

YANGA YAONDOLEWA KOMBE LA SHIRIKISHO NA WAARABU



Klabu ya nchini Algeria MC Alger imefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya kombe la shirikisho kwa vilabu barani Afrika baada ya kuifunga Yanga ya Tanzania mabao manne kwa bila katika mchezo wa marejeano uliopigwa April 15 nchini Algeria katika uwanja wa July 5 1962 mjini Al-Jaza’ir. Yanga ambao waliingia wakiwa wanahitaji sare ya aina yoyote ili waweze kupata nafasi ya kuingia katika hatua ya makundi ya Kombe la shirikisho kwa vilabu barani Afrika kutokana na ushindi wa goli moja walilolipata katika mchezo wa awali uliopigwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam April 8, wamejikuta wakikubali kipigo cha magoli 4-0 na safari yao kuishia hapo.


Magoli ya MC Alger ambao waliingia uwanja wa July 5 1962 wakiwa na sapoti kubwa ya mashabiki wao yalifungwa na Aouadj dakika ya 14 na 91, Derrardja dakika ya 39 na Zerdab dakika ya 66, hivyo Yanga wanaondolewa katika michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika kwa jumla ya magoli 4-1.


No comments