Header Ads

test

RAIS MAGUFULI ASUBIRIA RIPOTI YA WAFANYAKAZI 9000 WA SERIKALI WENYE VYETI FEKI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akizungumza katika hotuba yake ya Jumamosi ya April 15, 2017 katika uzinduzi wa majengo ya Hosteli za Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) yatakayo chukua wanafunzi 3,840, alisema kuwa anasubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa ambao wanatumia vyeti vya kufoji.



Pia Rais Magufuli alisema kumekuwa na changamoto kubwa katika kila sekta hivyo sasa anasubiri hiyo ripoti ili aweze kuifanyika kazi na kutenda haki katika jambo hilo.
“Naisubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa ambao wana vyeti vya kufoji ili niifanyie kazi” alisema Rais Magufuli
Aliongeza kusema, “Kwa hiyo mnaweza kuona shida zilizopo katika nchi hii, huku wafanyakazi hewa karibia 19000, mikopo hewa, wanafunzi ambao walikuwa ni hewa ni zaidi ya 56000. Kila mahali unapoenda kuna tatizo lakini ni lazima tuyatatue haya matatizo kwa sababu mlinichagua kwaajili ya matatizo haya,”.
Mwisho Rais aliwataka watanzania kufanya kazi kwa bidii na kuiunga mkono serikali katika harakati za kuwaletea maendeleo watanzania wa chini.


Tangaza Nasi kupitia Dawatihurutz.blogspot.com

No comments