Header Ads

test

BARUA YA KAGERA SUGAR TFF KUPINGA KUPOKWA POINTI TATU NA KAMATI YA SAA 72

TIMU ya Kagera Sugar ya Bukoba imetuma barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupinga uamuzi wa Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania, maarufu kama Kamati ya Saa 72 wa kuipa Simba SC pointi tatu na mabao matatu kutokana na Rufaa waliyoikatia timu hiyo kwa madai ya kumtumia beki Mohammed Fakhi akiwa ana kadi tatu za njano katika mechi baina ya timu hizo Aprili 2, mwaka huu.

Katika barua iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Kagera Sugar, Hamisi Madaki kuelekea kwa Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa, klabu hiyo imeliomba shirikisho hilo kupitia upya maamuzi ya Kamati ya Saa 72 kwa kuwa Fakhi hakuwa na kadi tatu za njano kama ilivyodaiwa.




Tangaza Nasi kupitia [dawatihurutz.blogspot.com]



No comments