Header Ads

test

FIFA NA CAF WAUKUBALI UWANJA WA CCM KIRUMBA MECHI ZA KIMATAIFA

Shirikisho la soka duniani, FIFA na lile la Afrika, CAF kwa pamoja wameupitisha uwanja wa CCM Kirumba uliopo jijini Mwanza, kutumika kwenye mechi za kimataifa.


Siku kadhaa zimepita tangu club ya Young Africans ikataliwe na shirikisho la soka Tanzania TFF kuutumia uwanja wa CCM Kirumba katika mechi yake ya Kombe la shirikisho dhidi ya MC Alger iliyochezwa April 8, 2017 uwanja wa Taifa badala ya CCM Kirumba kuwa hauna vigezo.

Habari hizo zimekuja baada ya Rais wa shirikisho la soka Tanzania, TFF, Jamal Malinzi ametweet katika ukurasa wake wa Twitter " Wana Mwanza hongereni Uwanja wa CCM Kirumba umepitishwa na CAF na FIFA kutumika kwa mechi za Kimataifa".




Viwanja vingine ambavyo CAF na FIFA imevipitisha kwa mechi za kimataifa nchini hadi sasa ni Amani wa Unguja, Zanzibar, Azam Complex na uwanja wa taifa wa Dar es Salaam.
Kupitishwa kwa CCM Kirumba kuna maana kuwa sasa mechi kubwa kama vile fainali za Kombe la Shirikisho, Ngao ya Hisani pamoja na mechi kubwa za kimataifa za kirafiki na mashindano ya CECAFA, CAF na FIFA ruksa kufanyika huko.
Viwanja vingine ambavyo vimekaguliwa na vinasubiri kupitishwa ni Gombani ulioko Pemba; Sokoine wa Mbeya na Kaitaba wa Kagera.


Tangaza Nasi kupitia [dawatihurutz.blogspot.com]


No comments