HABARI NJEMA: ROMA NA WENZAKE WAREJEA RASMI URAIANI
Msanii Roma na wenzake watatu walitekwa na watu wasiojulikana Alhamisi hii wakiwa Tongwe Record na mapema Jumamosi hii walionekana wakiwa oysterbay polisi.
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa Mwananyamala hospitali muda mchache baada ya kufanyiwa vipimo na kuachiwa huru, Roma alisema kwa sasa anaendelea vizuri pamoja na wenzake.
“Kutokana na mazingira na situation nzima hatutakuwa na muda mrefu zaidi wa kuongea zaidi ya dakika moja. Lakini niwahakikishie mimi ni mzima mpaka sasa hivi, niko njema kabisa, kiafya, kiakili na kivingine. Hata wenzangu watatu nikimaanisha, Moni, Bin Laden pamoja na Imma wote ni wazima” alisema Roma.
Aliongeza, Tuko katika taratibu za kutoa taarifa za tukio zima ambalo limetokea, taratibu hizo zinatufunga kwa sasa tushindwe kuzungumza. Lakini ratiba ambayo naweza kuwapatia Jumatatu nadhani tutakuwa na press conference kueleza nini kilitokea,”
Post a Comment