Header Ads

test

SIMBA YAFANYE KWELI DAKIKA ZA MWISHO DHIDI YA MBAO FC YA MWANZA


SIMBA SC imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya VodacomTanzania baada ya kushinda mchezo wao dhidi ya MBAO FC ya Mwanza uliofanyika leo katika dimba la CCM KIRUMBA MWANZA. MBAO FC ambao walikuwa wenueji waliweza kutawala mchezo huo dakika 45 za kipindi cha kwanza na kuweza kuongoza kwa magoli 2 mbele ya SIMBA SC ambao walikuwa wageni katika uwanja huo. 

Mabao ya mbao yalifungwa katika dakika ya 21 na George Sangija na lile lililofungwa dakika ya  36 na Evarigestus Bernard aliyemalizia pasi ya mfungaji wa bao la kwanza, Sangija.



Baada ya MBAO FC kupata bao la kwanza katika mchezo huo Kocha wa SIMBA SC Mcameroon Joseph Marius Omog  alifanya mabadiliko akimpumzisha mshambuliaji Pastory Athanas na kumuingiza kiungo Said Hamisi Ndemla. 


Mbao wakaendelea kutawala mchezo baada ya bao hilo na haikuwa ajabu dakika ya 36 walipopata bao la pili kupitia kwa Evarigestus Bernard aliyemalizia pasi ya mfungaji wa bao la kwanza, Sangija.


Baada ya bao hilo, kocha Omog wa Simba akamuinua mshambuliaji Mrundi Laudit Mavugo kwenda kuchukua nafasi ya beki wa kulia, Hamad Juma.

Simba wakafanya mabadiliko ya ndani, Bokungu akienda kucheza beki ya kulia na Mghana James Kotei akirudi kucheza beki ya kati na Mganda Juuko Murshid.

Kipindi cha pili, kocha Omog alikianza na mabadiliko tena akimtoa mshambuliaji Juma Luizio na kumuingiza Blagnon aliyekwenda kufanya kazi kubwa akicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi kuu mzunguko wa pili.

Blagnon alifunga bao la kwanza la Simba dakika ya 82 kwa kichwa kuparaza akiwa amelipa mgongo lango la Mbao kufuatia mpira mrefu wa James Kotei.

Bao hilo lilifungwa dakika tano tu baada ya Nahodha wa Mbao, Yussuf Ndikumana kuumia na kukimbizwa hospitali, nafasi yake ikichukuliwa na.

Blagnon tena akawainua vitini mashabiki wa Simba baada ya kufunga katika purukushani kwenye eneo la Mbao kufuatia mpira mrefu wa Bokungu dakika ya 91.
Katika mchezo huo uliodumu kwa dakika 103, kiungo Muzamil Yassin aliifungia Simba bao la ushindi dakika ya 96 akimalizia mpira uliorudi baada ya kuokolewa na mabeki wa Mbao.

Ushindi huo unairejesha Simba kileleni, ikifikisha pointi 58 baada ya kucheza mechi 26, wakati mabingwa watetezi, Yanga wanarudi nafasi ya pili kwa pointi zao 56.



Msimamo Ligi Kuu ya Vodacom 2016/2017:



No comments