Header Ads

test

KAULI ZA RAIS MAGUFULI WAKATI WA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASA DAR ES SALAAM - MOROGORO



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa reli ya kisasa standard gauge kutoka jijini Dar es Salaam hadi Morogoro. 





Hizi hapa kauli zake katika uzinduzi huo;

'Ujenzi wa reli huwa ni gharama kubwa, reli hii itakuwa inabeba uzito mkubwa na spidi kubwa, watu watalala Moro na watafanya kazi DSM'-Rais Magufuli

'Ujenzi wa reli ya kisasa utakuza sekta zingine nchini, itawezesha malighafi mbalimbali kusafirishwa kwenda kwenye maeneo ya viwanda'-Rais Magufuli

'Ujenzi wa reli hii ya kisasa utasaidia kutunza barabara zetu, barabara zetu zinaharibika kwa sababu zinasafirisha mizigo mikubwa'-Rais Magufuli

'Mradi huu wa ujenzi wa reli ya kisasa unatarajiwa kutoa ajira kwa watu takribani 600,000'-Rais Magufuli

'Mradi huu wa ujenzi wa reli ya kisasa unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 30'-Rais Magufuli 

'Wale wataalamu wa kusoma kwenye mitandao wakaangalie ni nchi gani imejenga reli ya namna hii kwa pesa zake watakuta ni Tanzania'-Rais Magufuli

'Unapokuwa dereva wa lori na unapopakia abiria hutakiwi kuwauliza wasimame waangalie sehemu gani, dereva mzuri anangalia kufika salama'-Rais Magufuli

'Nawahakikishia Watanzania mimi ni dereva mzuri nawahakikishia lori litafika kule tunakokwenda na hili ni lori la maendeleo'-Rais Magufuli

'Kazi tunazozifanya mara nyingi utakaowaona wanapiga kelele ni wale ambao walizoea kupiga dili, na mimi nataka waendelee kupiga kelele'-Rais Magufuli

'Tanzania imekuwa kwa uchumi 7%, ushahidi wa kukua kwa uchumi ndio hii miundombinu tunayoijenga'- Rais Magufuli

'Hivi karibuni tumepata mkopo wa kuanza kujenga barabara za mwendokasi katika awamu ya tatu na ya nne'-Rais Magufuli 

'Tunajua tunapoenda pasitokee mtu wa kubadilisha ajenda tuanze kuzungumzia ajenda ambazo hazipo kwenye ilani ya uchaguzi'-Rais Magufuli

'Nataka mhandisi amalize mradi wa reli ya kisasa kabla ya miezi 30, na ikiwezekana siku ya kufungua twende bure mpaka Dodoma'-Rais Magufuli

'Vita ya kupambana na ufisadi ni ngumu na hasa unapowabadilisha watu wachache waliozoea maisha fulani kwa miaka 50'-Rais Magufuli

'Wanasema samaki mkunje akiwa mbichi, fisadi mkunje akiwa mbichi akishakomaa mvunje, nafuu walalamike wachache, Watanzania wafurahi'-Rais Magufuli

'Nazuia hata michanga ya madini, ninafanya kazi hii kwa niaba yenu, kwani nashindwa kusema nipelekee hiyo michanga nitaikuta Ulaya?'-Rais Magufuli

'Mlinituma nifanye haya, au niwaulize ndugu zangu haya yote ninayoyafanya kweli ni mabaya?'- Rais Magufuli 

'Niko kwa niaba yenu, tumeonewa sana, Tanzania ni tajiri hatutakiwi kuwa ombaomba'- Rais Magufuli 

'Tanzania tunaweza kwa hiyo tunapoyafanya haya tunafanya kwa sababu tuna wajibu wa kufanya, na haya ni malipo yangu kwenu'-Rais Magufuli

'Watanzania wanataka maendeleo, hakuna anayekula siasa kwa hiyo Tanzania kwanza siasa baadae'-Rais Magufuli 


'Niwaombe tuangalie Tanzania kwanza siasa baadae, muiache Serikali ya CCM iliyoaminiwa na Watanzania itekeleze wajibu wake tutakutana 2020'-Rais Magufuli

No comments